Profesa Mbarawa amesema kuna sekta tatu muhimu ambazo ni moyo wa nchi ya Tanzania ambazo ni Barabara, Uchukuzi na Mawasiliano.
Barabara zijengwe kwa viwango..”Lazima TANROADS muwe katika kiwango cha juu, Serikali haitavumilia wafanyakazi wazembe, kwenye viwango vya barabara kila mtu atabeba msalaba wake, nikipata ripoti kama umefanya kosa tunakufukuza na kukufungulia mashtaka” Profesa Mbarawa.
Barabara isiyokuwa na kiwango lazima muhusika aondolewe.
Mizani kufanya malipo kwa njia ya Kielekroniki...”Mizani yetu lazima iwe ya kisasa, hatutaki kuona magari yanapanga foleni bila sababu, tunataka malipo yawe kwa kielektroniki ili tupunguze utumiaji wa fedha, tunataka tujue kinachoendelea kwa kuwa kuna baadhi ya wafanyakazi sio waaminifu, mtu akilipa pesa yake iweze kuingia moja kwa moja ofisini“..Prof.Mbarawa.
Tunataka mtu akilipia kila mtu anaona kwa uwazi kuanzia Wizarani, Tanroads kila mmoja aweze kuona kiasi kilicholipwa kwa sababu kuna baadhi ya wafanyakazi si waaminifu na kesi nyingi tumezisikia.
Uharibifu wa miundombinu..”Kuna changamoto kubwa sana wakati barabara zinajengwa, utakuta leo inajengwa na kuwekwa alama lakini kesho inavunjwa na baadhi ya watu, inabidi tutoe elimu kuanzia ngazi za chini, hatutakuwa na kigugumizi wala kumuonea huruma mtu yeyote ambaye atafanya makosa hasa kwenye viwango vya barabara”.
No comments:
Post a Comment